Nyimbo Za Dini Pamoja Na Nyimbo Za Watot (1983),
p. 4
Njooni, Njooni, Enyi Watakatifu
Njooni, Njooni, Enyi Watakatifu
1. Njooni enyi Watakatifu;Kwa moyo tembea.Safari yaweza kuwa ngumu,Neema yatosha.Ni bora tuvumilieWasiwasi tuondoe;Fanya hivi, mfurahi—Ni shwari! Ni shwari!
2. Je, tulijutie fungu letu?Si hivyo; ni sawa.Je, tuitegemee thawabu,Vitani twatega?Dhamiria; jipe moyo.Mungu wetu nasi yupo;Punde itanenwa hivi—Ni shwari! Ni shwari!
3. Tutayapata makao mapya,Sayuni tufike,Ambapo hatutasumbuliwa;Baraka tupate.Tutapaza nyimbo zetuKumsifu Mungu wetu;Na tutasema zaidi—Ni shwari! Ni shwari!
4. Na tukifa kabla ya kufika,Hakika! Ni shwari!Tutakuwa huru, bila shida,Tuishi peponi!Na kama tutakuwepoKuliona kimbilioTutaimba jinsi gani—Ni shwari! Ni shwari!