Number 15
Asubuhi Ile Njema
Asubuhi Ile Njema
1. Asubuhi ile njema!Jua likachomoza.Na sauti zao ndege,Zote zilisikika.Hapo katika kisituJoseph kamwomba Baba,Hapo katika kisituJoseph kamwomba Baba.
2. Alipopiga magoti—Sala yake ya kwanza—Nguvu za Shetani nazoZikamshambulia;Hakusita kuaminiMungu atamlinda,Hakusita kuaminiMungu atamlinda.
3. Ghafla mwanga ukashukaUnaozidi jua,Na mwale wa utukufuUkammulikia,Ndipo wakaja wawili,Mungu Baba na Mwana,Ndipo wakaja wawili,Mungu Baba na Mwana.
4. “Huyu, Mwanangu Mpendwa;Utamsikiliza!”Kajibiwa sala yake,Akamtii Bwana.Ni furaha iliyoje,Kumwona Mungu Baba,Ni furaha iliyoje,Kumwona Mungu Baba.
Maandishi: George Manwaring, 1854–1889
Muziki: Sylvanus Billings Pond, 1792–1871; umefanyiwa marekebisho na A. C. Smyth, 1840–1909