Number 30
Utukufu na Sifa
Utukufu na Sifa
1. Utukufu na sifaMfalme ni vyako,Wanao twakusifuHosana kwa Kristo.Bwana wa Israeli,Mwana wa Daudi,Unayekuja Yesu,Kama Mkombozi.
2. Kundi la malaikaLakusifu juu,Navyo viumbe vyoteVyatoa majibu.Kama WaebraniaWabeba matawi,Tunakupa upendoNa sifa, Mwokozi.
3. Kabla ya kifo chako,Waliimba sifa;Sasa upo mbinguni,Twakusifu Bwana.Pokea sifa zetu,Na pendo la kweli,Kwako yote ni mema,Mfalme mzuri.
Maandishi: Theodulph wa Orleans, 760–821
Muziki: Melchior Teschner, 1584–1635