1. Bwana, dhoruba yavuma!Mawimbi ni makali!Na giza limetanda mbingu.Hifadhi ipo mbali.Hujali twaangamia?Walalaje foo,Hali kila dakika yatishaNa tishio la kifo?
Upepo, mawimbi yaitika:Nyamaza.Ghadhabu ya tufani, iwePepo chafu, watu au chochote,Hakuna maji ya kumdhuruBwana wa bahari, nchi, mbingu.Vyote vitakuitikia:Nyamaza, tulia.Vyote vitakuitikia:Tulizana.
2. Bwana, kwa majonzi mengiLeo nanyenyekea.Moyo umejaa taabu.Niokoe, naomba!Mabubujiko ya dhambiYalemea roho,Nafa maji! Nazama! Ee Bwana.Ninyoshee mkono!
Upepo, mawimbi yaitika:Nyamaza.Ghadhabu ya tufani, iwePepo chafu, watu au chochote,Hakuna maji ya kumdhuruBwana wa bahari, nchi, mbingu.Vyote vitakuitikia:Nyamaza, tulia.Vyote vitakuitikia:Tulizana.
3. Bwana, vitisho vyakoma.Hali sasa tulivu.Jua la akisi ziwani,Moyoni sina hofu.Kawia, Bwana mpendwa!Nitoe upweke,Nifikie bandari ya kheriPwani nipumzike.
Upepo, mawimbi yaitika:Nyamaza.Ghadhabu ya tufani, iwePepo chafu, watu au chochote,Hakuna maji ya kumdhuruBwana wa bahari, nchi, mbingu.Vyote vitakuitikia:Nyamaza, tulia.Vyote vitakuitikia:Tulizana.
Maandishi: Mary Ann Baker, 1831–1921
Muziki: H. R. Palmer, 1834–1907