Number 71
Amri Zake Mungu
Amri Zake Mungu
1. Amri zake MunguNi njema hakika!Mtwike mzigo wako,Na atakutunza.
2. Kwenye lindo lake,Wema huwalea.Mkono wake mkuuWana huwalinda.
3. Mzigo wa hofu,Usikuangushe.Kimbilia kwake BabaNguvu upatiwe.
4. Wema wake kwetuHaubadiliki;Nitautua mzigo,Na nitafurahi.
Maandishi: Philip Doddridge, 1702–1751
Muziki: Hans Georg Nägeli, 1773–1836; umepangiliwa na Lowell Mason, 1792–1872