Number 88
Baki Nami; Kumekuchwa
Baki Nami; Kumekuchwa
1. Baki nami; kumekuchwa.Muda ni jioni;Giza sasa laingia;Haliepukiki.Moyoni mwangu, mwalikwa,Kaa nami kwangu.
Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.
2. Baki nami; kumekuchwa.Kuwapo pamojaKumegusa moyo wangu,Tulipoongea.Umejaza nafsi yanguKwa kuwa karibu.
Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.
3. Baki nami; kumekuchwa.Usiku mpwekeKama hutanena nami,Uniangazie.Giza, linanitishia,Kuingia kwangu.
Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.Mwokozi baki na mimi;Ona, kumekuchwa.
Maandishi: M. Lowrie Hofford, 1823–1888
Muziki: Harrison Millard, 1830–1895