1. Sasa kwa ustahifu,
Kwa upole sujudu.
Tathminia, wazia
Niliyokufanyia.
Kwa damu yangu nyingi,
Na maumivu mengi,
Kwa mwili wangu pia
Nimekushuhudia.
2. Mkate huu kwenu,
Ni kama mwili wangu;
Maji au divai,
Damu msalabani.
Nilichofanya, ewe
Mwanadamu usife,
Pale Fuvu la Kichwa,
Ni kifo kupitia.
3. Shauri moyo wako,
Tulia na nduguzo.
Wasamehe wengine
Hata nikusamehe.
Kwa sala ya imani
Shida zako kabidhi,
Na neema ya Roho
Iwe kisima kwako.
4. Kwenye Kiti cha Enzi,
Kwenu ni mtetezi;
Upendo wangu kwako,
Hata hauna mwisho.
Kuwa na utiifu,
Daima mwangalifu,
Kwangu uwe mwamini,
Kwako niwe Mwokozi.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: Ebenezer Beesley, 1840–1906