Number 104
Ona Mkombozi Afa
Ona Mkombozi Afa
1. Ona Mkombozi afa,Deni la haki kulipa.Afa dhabihu ya dhambi,Afa dhabihu ya dhambi,Ili tupate ushindi.
2. Mateso yake wabeza,Hata mbavu wamchoma;Kwa dharau na kebehi,Kwa dharau na kebehi,Miiba avikwa taji.
3. Akapatwa na matesoHakunung’unika neno.Wajibu atekeleza,Wajibu atekeleza,Na Baba amtukuza.
4. “Baba, ondoa kikombe,Upendavyo, ndivyo iwe.Nimefanya kazi yako,Nimefanya kazi yako;Ipokee yangu Roho.”
5. Alikufa; kwa uchungu,Jua likaficha nuru!Na kwa huzuni, dunia,Na kwa huzuni, duniaIkajibu, “Mungu afa!”
6. Aishi— aishi sasa,Mbele ya hizi ishara,Twaja kwa unyenyekevu,Twaja kwa unyenyekevu,Amri zake kuheshimu.
Maandishi: Eliza R. Snow, 1804–1887
Muziki: George Careless, 1839–1932