Number 111
Kafufuka!
Kafufuka!
1. Kafufuka! Kafufuka!Itangaze kwa shangwe.Kifungo chake kavunja;Watu wafurahie.Kifo kina ukomo,Ushindi ni wa Kristo.
2. Njoo na utakatifu;Sifu ushindi wake.Hakuna kiza cha winguKuzuia miale,Siku njema yaanza,Ishara ya Pasaka.
3. Kafufuka! Kafufuka!Amefungua mbingu.Dhambi haitatufunga,Tuna utakatifu.Na nuru ya PasakaMachoni itang’aa.
Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895
Muziki: Joachim Neander, 1650–1680