Number 116
Malaika wa Juu
Malaika wa Juu
1. Malaika wa juu
Makondeni waimba,
Na milima yajibu
Miwangwi ya furaha.
Utukufu kwake Mungu juu.
Utukufu kwake Mungu juu.
2. Wachungaji, kunani?
Mbona nyimbo mwaimba?
Ni taarifa gani
Zinazowavutia?
Utukufu kwake Mungu juu.
Utukufu kwake Mungu juu.
3. Njooni mumuone
Yule anayeimbwa;
Njoo, msujudie
Mtoto, Kristo Bwana.
Utukufu kwake Mungu juu.
Utukufu kwake Mungu juu.
Maandishi: Wimbo wa Krismasi wa Ufaransa, mnamo 1862
Muziki: Wimbo wa Krismasi wa Ufaransa