1. Wapendwa wa Mchungaji,\nNi kondoo wapendwa;\nTunu pendo awapalo,\nTunu kuliko fedha.\nWapendwa wa Mchungaji,\nNa kondoo “wengine”;\nMilimani awasaka,\nHata kina chochote.\n\n[Chorus]\nJangwani watangatanga,\nWasumbuka wapweke;\nAenda kuwakomboa,\nZizini warudishwe.\n\n2. Wapendwa wa Mchungaji,\nNdio wanakondoo;\nKuna wanaopotea,\nWadhoofika huko.\nOna, Mchungaji Mwema,\nAsaka wapotevu,\nAwarudisha kwa shangwe,\nNa kwa gharama kuu.\n\n[Chorus]\nJangwani watangatanga,\nWasumbuka wapweke;\nAenda kuwakomboa,\nZizini warudishwe.\n\n3. Wapendwa wa Mchungaji,\nNi “tisini na tisa.”\nApenda wapoteao,\nTumaini wakosa.\nSikia! Wito wa moyo,\nKwa upole asihi:\n“Hutafuti mpotevu,\nAliye mbali nami.”\n\n[Chorus]\nJangwani watangatanga,\nWasumbuka wapweke;\nAenda kuwakomboa,\nZizini warudishwe.\n\n4. Malisho yanavutia;\nMaji yenye uhai.\nBwana, kwa ari twajibu,\n“Ndiyo, tunakubali!\nTufanye wachunga wako;\nTupe pendo la kina.\nTutume mbali jangwani,\nKondoo kuwasaka.”\n\n[Chorus]\nJangwani watangatanga,\nWasumbuka wapweke;\nTwendeni kuwakomboa,\nZizini warudishwe.\n