1. Kuna nuru moyoni mwangu,
Ng’aavu tukufu,
Kuliko ya duniani.
Yesu mwanga wangu.
Kuna nuru na baraka,
Siku inapokuwa nzuri,
Akitabasamu Yesu,
Kuna nuru moyoni.
2. Kuna wimbo moyoni mwangu,
Kumsifu Bwana,
Na anasikia wimbo
Usioimbika.
Kuna nuru na baraka,
Siku inapokuwa nzuri,
Akitabasamu Yesu,
Kuna nuru moyoni.
3. Kuna upya moyoni mwangu,
Akiwepo Bwana,
Amani ipo rohoni,
Neema anipa.
Kuna nuru na baraka,
Siku inapokuwa nzuri,
Akitabasamu Yesu,
Kuna nuru moyoni.
4. Kuna shangwe moyoni mwangu,
Sifa na shukrani
Kwa baraka zake Mungu,
Hapa na mbinguni.
Kuna nuru na baraka,
Siku inapokuwa nzuri,
Akitabasamu Yesu,
Kuna nuru moyoni.
Maandishi: Eliza E. Hewitt, 1851–1920
Muziki: John R. Sweney, 1837–1899