Auto-scroll is most reliable with MIDI (computer-generated) audio.
Practice
Loading…
Tuambizane Mema Daima
1. Tuambizane mema daimaNyumbani au popote;Kama ndege kati ya mauaSauti zipokelewe.Yafariji kwenye majonzi,Yatutia moyo nguvu,Na penye wingu la huzuni,Huleta pendo ng’aavu.
Kila neno jema litatukumbusha,Labakia kama kito.Tuambizane mema daima;Yawa taswira ya moyo.
2. Kama mwale wa jua SayuniNafsi yanafurahisha;Kama kisima cha maji safi,Taratibu yatuwama.Hivyo kwa sauti karimu,Urafiki tuujenge,Mioyo iwe mikunjufuNa kufurahi popote.
Kila neno jema litatukumbusha,Labakia kama kito.Tuambizane mema daima;Yawa taswira ya moyo.