Number 133
Tenda Mema
Tenda Mema
1. Tenda mema; imeanza siku,Mwanga na uhuru vyaingia.Na malaika waandika juuKila tendo, hivyo tenda mema.
Tenda mema; matokeo badaye.Kwa nguvu uhuru pigania;Kwa moyo shupavu uendelee.Mungu yupo, hivyo tenda mema!
2. Tenda mema; zafunguka pingu.Wafungwa uhuru wamepata.Kwa imani hawana maumivu.Ukweli wasonga; tenda mema.
Tenda mema; matokeo badaye.Kwa nguvu uhuru pigania;Kwa moyo shupavu uendelee.Mungu yupo, hivyo tenda mema!
3. Tenda mema; uoga uache.Songa mbele, lengo waliona.Nayo machozi yatakwisha punde.Kuna baraka kutenda mema.
Tenda mema; matokeo badaye.Kwa nguvu uhuru pigania;Kwa moyo shupavu uendelee.Mungu yupo, hivyo tenda mema!
Maandishi: Hajulikani, The Psalms of Life, Boston, 1857
Muziki: George Kaillmark, 1781–1835