Number 140
Askari wa Kristo
Askari wa Kristo
1. Askari wa Kristo!Mwendo wa vita!Msalaba WakeWatangulia.Jemadari, Kristo,Ndiye Mshindi.Fuata bendera!Twende vitani.
Askari wa Kristo!Mwendo wa vita!Msalaba WakeWatangulia
2. Panapo ushindiShetani mbio;Askari tusonge,Ushindi bado.Adui huhofuShangwe za sifa;Ndugu, tuimbeni,Sauti paza.
Askari wa Kristo!Mwendo wa vita!Msalaba WakeWatangulia.
3. Kanisa la MunguNi jeshi kuu;Ndugu, tunapitaPatakatifu.Hatugawanyiki;Ni moja umbo;Katika hisaniNa mafundisho.
Askari wa Kristo!Mwendo wa vita!Msalaba WakeWatangulia.
4. Mbele basi watu,Jumuikeni.Sauti ziimbeKama washindi:Sifa na adhamaKwake Mfalme.Hivyo malaika,Watu, waimbe:
Askari wa Kristo!Mwendo wa vita!Msalaba WakeWatangulia.
Maandishi: Sabine Baring-Gould, 1834–1924
Muziki: Arthur S. Sullivan, 1842–1900