1. Tumaini la Sayuni,
Kizazi cha ahadi,
Ona, Bwana aamuru,
Pambaneni vitani!
Israeli, simama,
Onya, “Chunga na omba!”
Angamiza adui
Na upanga wa haki.
2. Ona wingi wa adui,
Kwenye safu za dhambi.
Israeli tupambane;
Tusikose ushindi!
Israeli, simama,
Onya, “Chunga na omba!”
Angamiza adui
Na upanga wa haki.
3. Sayuni, pinga maovu
Kwa haki na upanga!
Tuzizime mbinu zote,
Twendelee kushinda.
Israeli, simama,
Onya, “Chunga na omba!”
Angamiza adui
Na upanga wa haki.
4. Punde vita vitaisha;
Adui, chini yenu.
Songa wana wa Sayuni;
Taji, yenu thawabu.
Israeli, simama,
Onya, “Chunga na omba!”
Angamiza adui
Na upanga wa haki.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: William Clayson, 1840–1887