1. Sikilizeni, mataifa!
Shangilieni kwa pamoja,
Malaika imbeni wimbo:
Nuru tena ipo!
Injili, mwanga wa ukweli,
Wan’gara kutoka mbinguni,
Ni mng’aavu kama jua
Kote waangaza.
2. Watu walisaka gizani,
Wakakesha wakisubiri.
Sasa usiku umekwisha,
Nuru yarejeshwa!
Injili, mwanga wa ukweli,
Wan’gara kutoka mbinguni,
Ni mng’aavu kama jua
Kote waangaza.
3. Tumeitwa na Mungu wetu ,
Kutumikia wote watu,
Tutasimamia ukweli,
Neno kuhubiri.
Injili, mwanga wa ukweli,
Wan’gara kutoka mbinguni,
Ni mng’aavu kama jua
Kote waangaza.
Maandishi: Kutokana na maandishi ya Kijerumani na Louis F. Mönch, 1847–1916. © 1985 IRI
Muziki: George F. Root, 1820–1895