Number 153
Yehova, Bwana wa Wote
Yehova, Bwana wa Wote
1. Yehova, Bwana wa wote,
Tangaza ukweli,
Uenee pande zote,
Na waukubali;
Uenee pande zote,
Na waukubali.
2. Kanisa lako likue,
Ufalme wa Mungu,
Na amani duniani
Iakisi mbingu.
Na amani duniani
Iakisi mbingu.
3. Kazi isogee mbele
Kwayo mataifa,
Yakawe kwenye ufalme,
Na ukawe Bwana,
Yakawe kwenye ufalme,
Na ukawe Bwana.
4. Ndipo wanadamu wote
Watakuimbia,
Watasalimu mawingu,
Wote wataimba;
Watasalimu mawingu,
Wote wataimba.
Maneno: Hajulikani
Muziki: Oliver Holden, 1765–1844