Number 158
Fimbo Ya Chuma
Fimbo Ya Chuma
1. Kwa Nefi, mwonaji yule,Mungu kafunua,Mfano wa neno lakeNi fimbo ya chuma.
Ishike fimbo ya chuma;Aminifu kweli.Hii fimbo— neno la Bwana—Mwongozo thabiti.
2. Tupo bado safarini,Kwenye majaribu;Tutapitia gizani,Penye hatari tu.
Ishike fimbo ya chuma;Aminifu kweli.Hii fimbo— neno la Bwana—Mwongozo thabiti.
3. Adui akisogea,Kutisha njiani,Tushike fimbo ya chuma,Tuombe auni.
Ishike fimbo ya chuma;Aminifu kweli.Hii fimbo— neno la Bwana—Mwongozo thabiti.
4. Hatua na kwa hatua,Siku hadi siku,Kwa sala na wimbo pia,Tusonge mbele tu.
Ishike fimbo ya chuma;Aminifu kweli.Hii fimbo— neno la Bwana—Mwongozo thabiti.
5. Pumziko li karibu,Yaongoza fimbo,Tutapata utukufuTukishika neno.
Ishike fimbo ya chuma;Aminifu kweli.Hii fimbo— neno la Bwana—Mwongozo thabiti.
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: William Clayson, 1840–1887