1. Nyimbo za moyoni
Sote tutaimba
Kwa pamoja nyumbani kwetu,
Huko tutaishi
Bila kutengana,
Daima na wapendwa wetu!
Huko tutaishi,
Nyimbo za moyoni
Tutaimba nyumbani kwetu.
2. Furaha ni yetu
Haielezeki,
Tutaimba mara kwa mara.
Tukiwapa busu,
Na kuwafariji
Ndugu waliotangulia.
Tukiwapa busu,
Furaha ni yetu,
Ndugu waliotangulia.
3. Tutaona mengi,
Huko selestia,
Na hayaelezeki kamwe.
Roho zitakiri
Wingi wa furaha
Katika nyimbo zenye shangwe.
Roho zitakiri,
Tutaona mengi
Katika nyimbo zenye shangwe.
4. Nyimbo gani bora
Na ukaribisho
Twapata pendo likijiri!
Tukiwa na raha
Na tuwapendao
Kwa wazazi wetu mbinguni!
Tukiwa na raha,
Nyimbo gani bora,
Kwa wazazi wetu mbinguni!
Maandishi: Joseph L. Townsend, 1849–1942
Muziki: William Clayson, 1840–1887