Number 170
Wazee wa Israeli (Wanaume)
Wazee wa Israeli (Wanaume)
1. Wazee wa Israeli twendeniPopote tuwasake wenye haki,Penye jangwa, bahari na misitu,Tuwalete Sayuni wawe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;Milima ya Efraemu twaenda.
2. Mavuno mengi wavunaji haba;Tukiungana yote twayaweza.Tutenganishe nganona maguguToka kifungoni wawekwe huru.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;Milima ya Efraemu twaenda.
3. Tuwatembelee nao maskiniWenye njaa na wale wenye dhiki;Tuwafariji kwa injili yakeTuwaonyeshe njia ya milele.
O! Babiloni, Babiloni twakuaga;Milima ya Efraemu twaenda.
Maandishi: Cyrus H. Wheelock, 1813–1894
Muziki: Thomas H. Bayly, 1797–1839, umefanyiwa marekebisho