1. Kwa kila ua dogo,
Ndege wa kuimba,
Kawapa rangi nzuri,
Kawapa na mbawa.
Vyote vyenye uzuri,
Miti na wanyama,
Vyote vyenye fahari
Bwana kaviumba.
2. Kilele cha mlima,
Mto wamwagika,
Jua lichomozapo
Huangaza anga.
Vyote vyenye uzuri,
Miti na wanyama,
Vyote vyenye fahari
Bwana kaviumba.
3. Upepo wa baridi,
Kiangazi chema,
Matunda bustanini,
Kayatengeneza.
Vyote vyenye uzuri,
Miti na wanyama,
Vyote vyenye fahari
Bwana kaviumba.
4. Miti yenye kijani,
Konde zavutia,
Kando kando ya maji
Tunakusanyika.
Vyote vyenye uzuri,
Miti na wanyama,
Vyote vyenye fahari
Bwana kaviumba.
Maandishi: Cecil Frances Alexander, 1818–1895
Muziki: Tuni ya Kingereza ya Kale. Umepangiliwa © 1989 IRI