1. O! Kisima cha baraka,
Imbisha moyo wangu;
Tiririko za rehema,
Zaniita kusifu.
Nifundishe tenzi nzuri,
Ziimbwazo uliko;
Mlima – wangu msingi —
Nasifu pendo lako.
2. Naita Ebenezeri,
Hapa nimefikia,
Nako kwa yako mapenzi,
Nyumbani nitafika.
Kupotea ni mwepesi,
Hata kumwacha Mungu;
Moyo wangu, Ee Mwokozi,
Ufunge kwako juu.
3. Alinitafuta Yesu
Nikiwa ugenini;
Akamwaga yake damu
Kunitoa jangani.
Kupotea ni mwepesi,
Hata kumwacha Mungu;
Moyo wangu, Ee Mwokozi,
Ufunge kwako juu.
4. O! Yanilazimu kuwa
Daima mwiwa wako!
Ufungavyo wako wema,
Nifunge wangu moyo.
Kupotea ni mwepesi,
Hata kumwacha Mungu;
Moyo wangu, Ee Mwokozi,
Ufunge kwako juu.
Maandishi: Robert Robinson, 1735–1790
Muziki: John Wyeth, 1770–1858