Page 12
Njooni Enyi Watoto Wa Bwana
Njooni Enyi Watoto Wa Bwana
1. Enyi wana wa Bwana,Tuimbe kwa umoja.Tupaze wetu wimboKwake atawalapo.Tutasafishwa wote,Na makosa yafutwe,Tutapoacha dhambi,Tuishi kwa amani.
2. TutakavyofurahiTumwonapo Mwokozi!Aja kwa utukufu,Kukomesha maovu.Nyimbo tutamwimbiaMfalme wetu, Bwana.Tutajaa upendo,Woga kufika mwisho!
3. Tutakuwa wasafi,Tutaishi nuruni.Tutamwimbia sifa;Shangwe tutazipaza.Dunia isafishweViumbe vyake vyote,Viishi kwa upendo;Furaha kila moyo.
Maandishi: James H. Wallis, 1861–1940
Muziki: Lahani ya Uhispania; umepangiliwa na Benjamin Carr, 1768–1831