Auto-scroll is most reliable with MIDI (computer-generated) audio.
Practice
Loading…
Roho wa Mungu
1. Roho wa Mungu awaka kama moto!Utukufu wa zama hizi waja;Zarudi baraka za kale, maono,Na malaika wazuru dunia.
Tutaimba nao majeshi ya mbinguHosana, hosana Mungu na Kristo!Utukufu wapewe walio juuSasa na milele yote, Amina!
2. Bwana atuongezea ufahamu,Kama mwanzo, mwamuzi arejeshwa.Waongezeka na uwezo wa Mungu;Pazia linaanza kupasuka.
Tutaimba nao majeshi ya mbinguHosana, hosana Mungu na Kristo!Utukufu wapewe walio juuSasa na milele yote, Amina!
3. Kusanyiko la kiroho tutaita,Na kueneza ufalme wa mbingu,Kwa imani tutaanza kurithishwaBaraka na utukufu wa Mungu.
Tutaimba nao majeshi ya mbinguHosana, hosana Mungu na Kristo!Utukufu wapewe walio juuSasa na milele yote, Amina!
4. Siku ya ajabu watakapolalaKondoo na simba bila ghadhabu,Efrahimu Sayuni kutunukiwa,Kwa garimoto ashukapo Yesu!
Tutaimba nao majeshi ya mbinguHosana, hosana Mungu na Kristo!Utukufu wapewe walio juuSasa na milele yote, Amina!
Maandishi: William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835. Yaliimbwa wakati wa kuweka wakfu, Hekalu la Kirtland mwaka 1836.