Number 8
Kwa Milima Twakutukuza
Kwa Milima Twakutukuza
1. Kwa milima twakutukuzaEwe, Mungu wetu;Unatuwezesha sanaKatika kazi zetu.Waileta IsraeliKwenye nchi yao.
Kwa milima twakutukuza,Ewe, Mungu wetu.
2. Mikononi mwa waonevuTumenyanyasika;Umekuwa msaadaWa kutuimarisha,Tukapita maaduiKatikati yao.
Kwa milima twakutukuza,Ewe, Mungu wetu.
3. Umetuongoza salamaHadi kwenye kingaUkiwa mlinzi wetuTangu tulikotoka.Kwa ajili ya miamba,Mabonde, na mito,
Kwa milima twakutukuza,Ewe, Mungu wetu.
4. Sisi twauchunga mnaraNuru isizime;Sisi ni waangaliziChini ya anga kete.Miamba yajasirisha,Kwa ya kwako fimbo;
Kwa milima twakutukuza,Ewe, Mungu wetu.
Maandishi: Felicia D. Hemans, 1793–1835; yamefanyiwa marekebisho na Edward L. Sloan, 1830–1874
Muziki: Evan Stephens, 1854–1930