Number 77
Hamu ya Nafsi ni Sala
Hamu ya Nafsi ni Sala
1. Hamu ya nafsi ni sala,Usemi halisi,Kama moto, ni hisia,Yawaka moyoni.
2. Pumzi hushushwa na sala,Hufuta machozi.Macho juu hutazamaKwa Mungu Mwenyezi.
3. Lugha nyepesi ni sala,Hata kwa mtoto.Wimbo unaovutiaMfalme alipo.
4. Sala kweli ni uhai;Kwa mkristo, hewa.Mlangoni mwa mautiHuenda kwa sala.
5. Sauti ya mwenye dhambi,Akianza toba,Malaika wafurahiKila akiomba.
6. Watakatifu makiniKupitia sala,Waupata ushirikiWa Baba na Mwana.
7. Tuombapo, si sisi tu;Na Roho aomba,Na Yesu kitini juuAnatuombea.
8. Ewe uliye Ukweli,Njia na Uzima.Uyajuaye maombiTufunze kuomba.
Maandishi: James Montgomery, 1771–1854
Muziki: George Careless, 1839–1932