Number 76
Sala ya Faragha
Sala ya Faragha
1. Kuna muda mtulivu,Pasipo karaha;Mbele ya Bwana nasaliSala ya faragha.
Moyo na ugeuke,Kuomba siku zote,Na ili nafsi yanguIungane na mbingu.
2. Njia nyofu ya mbinguni,Wapo malaika,Twaipata tufanyapo,Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke,Kuomba siku zote,Na ili nafsi yanguIungane na mbingu.
3. Dhoruba nipitiapo,Ni faraja kwamba,Bwana husikia ile,Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke,Kuomba siku zote,Na ili nafsi yanguIungane na mbingu.
4. Adui anitegapo,Mwokozi namwita,Huja kama nitasali,Sala ya faragha.
Moyo na ugeuke,Kuomba siku zote,Na ili nafsi yanguIungane na mbingu.
Maandishi na muziki: Hans Henry Petersen, 1835–1909